• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Urejelezaji wa Taka Ngumu

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatambua ongezeko la aina tofauti za taka ngumu zikiwemo za taka za majumbani, taka za viwandani na taka za Hospitali ambazo hutupwa maeneo mbalimbali na hivyo kuweza kusababisha uchafuzi wa mazingira (hewa, maji na Ardhi).

Jiji la Dar es Salaam linakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani 4,252 za taka kwa siku. Kati ya hizo ni asilimia 45 hadi 50 tu zinazopokelewa katika dampo sawa na tani 1,200 – 2,000 ya taka zinazokisiwa kuzalishwa kwa siku ambapo taka zinazobaki huishia kwenye maeneo ya wazi, mitaro ya maji, barabara na makazi.

Hali ya usafi wa Jiji la Dar es Salaam hususani udhibiti taka ngumu ni tatizo la muda mrefu ambalo lina changamoto nyingi. Tabia iliyozoeleka miongoni mwa jamii ya utupaji ovyo wa taka katika maeneo yasiyositahili imechangia Jiji kuwa chafu. Kuzagaa kwa taka kunaweza kuwa kichocheo cha milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu na magonjwa mengine ya kuhara na kutapika. Hali ya uchafu Jijini inachangiwa pia na elimu ndogo juu ya usafi wa mazingira, kutotii sheria zilizopo kwa upande wa wananchi na usimamizi hafifu wa sheria za usafi wa mazingira.

Ili kupunguza uchafuzi wa mazingira, Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeandaa sera ya urejelezaji wa taka ngumu ambayo itakuwa ni msingi muhimu kwa Taasisi za Serikali kuanza kutambua na kurasimisha sekta ya urejelezaji taka ambayo awali ilikuwa ikiendeshwa na Taasisi binafsi na vikundi visivyokuwa rasmi.

Katika kuhakikisha hilo linafanyika Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam inalenga kufanya yafuatayo;

  1. Kubuni miradi mbalimbali ndani ya Jiji itakayohusisha wadau mbalimbali inayolenga urejelezaji taka pamoja na masoko ya uhakika ya taka zilizorejelezwa au bidhaa zilizotokana na taka rejea.
  2. Kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kurejeleza taka ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Halmashauri za Manispaa katika kuhakikisha utenganishaji wa taka unafanyika kuanzia ngazi za uzalishaji (sorting at source).
  3. Kuwatambua na kuwaunganisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na teknolojia za urejelezaji taka ndani ya Jiji la Dar es Salaam
  4. Kutenga maeneo ya Viwanda vidogovidogo au karakana (recycling facility) ndani ya dampo au katika maeneo yake ambayo yatafaa kwa kazi zinazohusiana na urejelezaji taka.
  5. Kuhamasisha teknolojia zinazolenga uzalishaji na utumiaji wa bidhaa zitokanazo na taka rejea.
  6. Kuhakikisha inaweka mazingira bora yatakayowezesha ukuaji wa sekta ya urejelezaji taka ngumu kwa kuongeza viwanda na ubora wa bidhaa zake ili ziweze kupata soko ndani na nje ya nchi na hatimaye kukuza pato jamii na Taifa.
  7. Kuwezesha wananchi wa maisha ya chini wakiwemo vijana na wanawake kushiriki katika ubunifu na utumiaji wa teknolojia za urejelezaji taka na hatimaye kuweza kuboresha usafi.

Urejelezaji wa taka una faida nyingi miongoni mwa jamii kama; kuongeza thamani ya taka na kipato katika jamii, kupunguza malundo ya taka katika mitaa na maeneo ya jamii, kupunguza gharama za uendeshaji wa dampo, kupunguza gharama za udhibiti taka katika Manispaa na kuongeza uelewa wa jamii katika uchambuzi wa taka kuanzia ngazi ya kaya.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inalenga kuhakikisha kiwango cha juu cha uzuiaji wa uchafuzi wa mazingira kwa kuweka taratibu zitakazowezesha aina nyingi za taka zinatakazozalishwa katika Jiji ziweze kurejelezwa (Recycling and Re-use) ili kuwa na Jiji safi.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.