Na Doina Mwambagi
Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 19 Novemba, 2024 limepokea ujumbe wa Kamati ya kuthibiti UKIMWI kutoka Manispaa ya Kigamboni waliofanya ziara ya kujifunza mbinu mbalimbali za kuthibiti maambukizi ya UKIMWI ambapo walitembelea Kituo cha Afya Buguruni, Peer to Peer group iiiyopo Vingunguti pamoja na konga, ujumbe ulioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Stephano Waryoba.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mhe. Waryoba amewashukuru viongozi na watendaji wa Jiji la DSM kwa kukubali kuwapatia mafunzo hayo na kuwapongeza Watumishi wa Kituo cha Afya Buguruni kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa licha ya kuwa na changamoto ya uchache wa watumishi.
Awali akiongea na ugeni huo, Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Ojambi Masaburi amesema “Nachukua nafasi hii kuwakaribisha katika Jiji la Dar es Salaam na tumefarijika kupokea ugeni huu mkubwa hii inatupa uwezo wa kubadilishana uzoefu, sisi tuwape yetu lakini pia tupokee kutoka kwenu.”
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa ikipokea wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaokuja kujifunza namna inavyotekeleza majukumu yake na kupata mafanikio.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.