Idara ya Ujenzi imegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni:-
Sehemu ya Barabara chini ya Mhandisi wa Barabara na Mhandisi wa Mitambo, husimamia na kusanifu miradi ya ujenzi, ukarabati na kuratibu matengenezo ya barabara na kufanya matengenezo ya magari na mitambo ya Halmashauri ya Jiji, Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam na Taasisi za watu binafsi. Barabara hizi ni zile zinazohudumiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Dampo la Pugu Kinyamwezi.
Sehemu ya Majengo na Miliki chini ya usimamizi wa Mhandisi wa Majengo hushughulikia usanifu, ujenzi, kazi za umeme na matengenezo ya nyumba, kumbi na Ofisi zote za Halmashauri ya Jiji, Dampo la Pugu Kinyamwezi, Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT) na soko la wafanya biashara ndogo ndogo la Ilala Business Park maarufu kama Machinga Complex.
Kila sehemu imepangiwa majukumu yake kiutekelezaji yanayokamilisha majukumu ya Idara ya Ujenzi ambayo ni pamoja na kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji juu ya mambo yote yanayohusu Uhandisi (Ujenzi na Mitambo)
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.