Thursday 2nd, January 2025
@Zakhem Mbagala
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda anapenda kuwakaribisha wananchi wote wa Jiji la Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya FURAHA YANGU itakayozinduliwa tarehe 07 Septemba, 2018 katika viwanja vya Zakhem Mbagala.
Kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo “PIMA, JITAMBUE, ISHI” inalenga kuongeza utambuzi wa Virusi vya UKIMWI (VVU) na kuanza dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI Mapema iwezekanavyo.
Katika uzinduzi huo huduma mbalimbali za Afya zitatolewa bila malipo yoyote ambapo kutakuwa na upimaji wa Virusi vya UKIMWI, Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi, na Magonjwa yasiyoambukiza. Aidha, wananchi watapata nafasi ya kuchangia damu.
Huduma zote hizo zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 05 Septemba, 2018 hadi tarehe 07 Septemba 2018 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.
WITO: Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaombwa kujitokeza kwa wingi HASA WANAUME katika kampeni hii ya FURAHA YANGU ili kuzijua vyema Afya zetu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.