JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Tarehe: 18 March, 2016

Mahali: City Hall

Muda: 08:00 - 15:30

Maelezo Ya Tukio:

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

ULIPAJI WA USHURU WA HUDUMA ZA JIJI “CITY SERVICE LEVY” KWA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA JIJINI DAR ES SALAAM

ROBO YA TATU YA JANUARI HADI MACHI 2016

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM ANAYATANGAZIA MABENKI YOTE NA TAASISI ZA FEDHA ZILIZOPO DAR ES SALAAM KUANDAA MALIPO YA KODI ZA HUDUMA ZA JIJI “CITY SERVICE LEVY” KWA ROBO YA TATU YA MWAKA AMBAYO NI JANUARI HADI MACHI 2016.

KWA MUJIBU WA SHERIA YA FEDHA YA SERIKALI ZA MITAA YA MWAKA 1982 NA KWA MUJIBU WA SHERIA NDOGO ZA “USHURU WA HUDUMA” ZA JIJI, 1997 MABENKI YANAPASWA KULIPA (0.2%) YA MAUZO GHAFI “GROSS TURNOVER” BAADA YA KUTOA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI NA KODI YA MLAJI.

USHURU HUU UNAPASWA KULIPWA KABLA YA TAREHE 05 APRILI, 2016. AIDHA KUSHINDWA KULIPA KWA WAKATI RIBA YA ASILIMIA 1.5 ITATOZWA KWA KILA MWEZI PAMOJA NA USHURU UNAODAIWA.

LIPA USHURU WA HUDUMA NDANI YA WAKATI KUEPUKA USUMBUFU UNAOWEZA KUJITOKEZA.

 

MALIPO YAFANYIKE BENKI YA CRDB PLC:

Jina la Akaunti

:

Dar es Salaam City Council

Akaunti Namba

:

0150211141600

Jina la Benki

:

CRDB Bank Plc

Jina la Tawi

:

Azikiwe Premier – Benjamin William Mkapa Tower

Swift Code

:

CORUTZTZ, Bank Key: 67034906

  Imetolewa na:

Wilson Kabwe

MKURUGENZI WA JIJI

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM