Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapandisha vyeo Watumishi zaidi ya elfu nne (4000) wa Jiji hilo ili waweze kupata hamasa katika utendaji kazi wao.
Mkurugenzi Mabelya ameyasema hayo Leo tarehe 5 Septemba, 2024 Ofisini kwake mara baada ya kumkabithi tuzo Afisa Utumishi Aisha Ally kwa kuratibu vizuri zoezi la kupandisha vyeo vya watumishi mwaka huu ambapo amesema Afisa huyo anastahili kupewa Tuzo hio kutokana na utendaji kazi Bora.
Amesema katika kutekeleza majukumu ya Serikali, Jiji la DSM limekuwa mfano wa kuigwa kwenye nyanja mbalimbali ili kutimiza adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda maslahi ya Watumishi na kuleta Maendeleo hapa Nchini.
Aidha, Mabelya amewataka Watumishi wa Jiji hilo kuhakikisha wanafanya kazi Kwa weledi ili kufikia malengo ya Serikali na kuwa mfano wa kuigwa katika utendaji kazi bora.
Nae Afisa Utumishi Aisha Ally amemshkuru Mkurugenzi kwa kumkadhi tuzo hio na kuaahidi kutoa ushirikiano kwa Watumishi wenzake katika utendaji kazi wao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.