Na,Amanzi Kimonjo.
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam leo Machi 2, 2022 imefanya Mkutano wa Baraza la Madiwani na kuweza kupitia taarifa mbalimbali za utendaji kazi zinazofanywa na Jiji hilo,Mkutano huo umefanyika ukumbi wa mikutano wa Anatoglou uliopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.Baraza hilo la madiwani limepitia taarifa ya utendaji kazi ya robo ya pili kutoka Oktoba hadi Disemba 2021 na kuweza kuangalia utendaji kazi huo katika kamati mbalimbali kama vile kamati ya fedha na utawala,uchumi na Huduma za Jamii,Mipango miji na Mazingira,pamoja na kamati ya kudhibiti UKIMWI pia kikao kimeweza kupitia taarifa hiyo ya utekelezaji wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba-Disemba 2021.Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam akizungumzia mradi wa Maendeleo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa iliyopo katika kata ya vingunguti Mhe.Omari Kumbilamoto amesema "mradi wa ujenzi wa machinjio ni mradi unausimamiwa usiku na mchana pamoja na genereta tayari limenunuliwa na kuhakikisha kazi zinaendelea kufanyika mpaka kufikia hatua iliyopo"Vilevile Mradi wa machinjio ya Vingunguti umekuwa mradi mkubwa katika Halmashauri ya Jiji kulingana na mahitaji ya machinjio hiyo ya kisasa ikiwa ni miungoni mwa hoja za maendeleo zilizoongelewa katika baraza hilo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi.Tabu Shaibu amesema "Mradi wa machinjio ya kisasa unaendelea na maagizo ya kamati ya fedha kuwa mradi huo ndani ya miezi mitatu kutoka machi hadi july kuweza kufikia hatua ya kukamilika".Katika upande wa maendeleo ya jamii ukamirifu wa madawati katika madarasa ya UVIKO uwepo wa madawati na ubora wa majengo hayo kuwa madarasa yamekamilika katika ubora pia suala la madawati ya kila darasa ni maagizo kutoka serikali kuu kuwa kila darasa lazima liwe na madawati hamsini hivyo basi madarasa yako na madawati mwenyekiti wakamati ya maendeleo ya jamii ambaye ni diwani wa kata ya Kipunguni Mhe.Mushi amesema "kila darasa moja la UVIKO likikamilika kwa maeneo yote tambalale basi ni lazima madawati Hamsini 50 yawepo tayari pindi mradi unapomalizika kwa ajili ya wanafunzi husika kukalia na kuendelea na masomo" sambamba na hilo pia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri wa Dar es Salaam Bi.Tabu Shaibu amesema" kufikia leo jioni shule ya Buguruni moto jumla ya Madawati 300 yamepelekwa kwa ajili ya kukamilika na kuendelea kuendeleza jukumu la kutoa elimu linaendelea".Pia,katika kikao hicho Afisa takukuru aliweza kutoa mafunzo kwa madiwani juu ya umuhimu wa usimamizi wa madiwani katika shughuli za maendeleo na kuweza kupanua mawazo na fikra ikiwemo uelewa juu ya masuala ya rushwa na viashiria vyake katika usimamizi wa miradi ya maendeleo katika kila kata Afisa TAKUKURU amesema Miradi hii ya maendeleo ipo kwenu madiwani na niwajibu kwenu kuweza kuisimamia ili kuona utendaji wa kazi thabiti unaendelea na kuona fedha za serikali zinatumika kikamilifu"Kamati ya ukimwi katika kipindi cha mwezi oktoba hadi kumekuwa na changamoto katika kudhibiti UKIMWI kwani changamoto kubwa ni sambamba na uwepo wa madangulo yanayohamasisha ngono zembe na kisababisha ueneaji wa ugonjwa wa UKIMWI Mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI Bi.Lucy amesema elimu inatolewa na pia semina zitatolewa kwa madiwani juu ya matumizi sahihi ya mipira na wananchi kupitia nyinyi madiwani mhamasishe watu waendelee kujikinga na UKIMWI kwani UKIMWI upo juma tatu hadi juma pili.Kwa kuhitimisha Madiwani wamepongeza juu ya ujio wa Afisa wa TAKUKURU katika kikao cha baraza la madiwani na kuweza kutoa mafunzo mazuri kwa madiwani juu ya usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kusema siku zote walisikia salamu kutoka TAKUKURU ila leo tumefurahishwa na ujio wenu tunawapa hongera na tunashukuru .
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi: 0713614364
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.