• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

CPA Makalla aagiza miradi ya maendeleo kukamilishwa kwa wakati

Tarehe iliyowekwa: July 9th, 2024

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM wa Taifa, CPA Amos Makalla, amewataka wakandarasi kukamilisha miradi kwa wakati huku akiwahimiza watendaji kuhakikisha wanasimamia kwa kasi utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili ikamilike kwa wakati.

CPA Makalla ametoa maagizo hayo leo Julai 09, 2024 Jijini Dar es Salaam akihitimisha ziara yake ya siku tatu katika Jimbo la Ilala ambapo alitembelea mradi wa ujenzi wa madarasa 20  ya ghorofa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja  wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 pamoja na Mradi wa barabara zaidi ya 20 zinazotekelezwa katika Mitaa mbalimbali za Kata ya Ilala  ikiwemo Mtaa wa Mwanza na Kigoma zitakazogharimu takribani shilingi bilioni 30 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu na fedha kutoka mradi wa DMDP.

Akiongea wakati wa ziara hiyo CPA Makalla ameeleza kuwa “Dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassani ni kuhakikisha anaboresha miundombinu yote kuanzia afya, elimu hadi barabara hivyo niwatake watendaji msimamie miradi hii kwa ukaribu ili ikamilike kwa wakati kwani fedha zipo. Pia niwatake wakandarasi kuhakikisha mnakamilisha ujenzi haraka kwani kupitia miundombinu hii tutakua tumetimiza dhamira ya Mhe. Rais ya kuboresha sekta ya elimu na miundombinu ya barabara”.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika Wilaya ya Ilala za utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Ilala kuboreshewewa mazingira ya biashara kwani Jiji la Dar es Salaam limetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa masoko makubwa ya kisasa yatakayoenda kumaliza changamoto zote wanazozikabili.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura ameahidi kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ikamilike kwani fedha za kukamilisha miradi hizo zipo japo wakandarasi ndio wanachangamoto ila atahakikisha changamoto hizo anazitatua na miradi itakamilika kwa wakati.




Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.