• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

DC Ludigija awataka Watendaji wa Mitaa kusimamia majukumu yao

Tarehe iliyowekwa: July 21st, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ngw'ilabuzu Ludigija  leo tarehe 21Julai, 2022 amefanya kikao kazi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lengo likiwa ni kuwakumbusha watendaji hao wanahakikisha wanasimamia majukumu yao kwa kuhakikisha wanadhibiti zoezi la biashara holela, wanasimamia usafi pamoja na kuhakikisha maegesho ya bajaji, bodaboda na guta zinazoingia katikati ya Mji wanaegesha vyombo hivyo katika vituo maalumu walivyopangiwa.

Kikao kazi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Arnatoglou uliopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kilihudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Jiji la DSM watendaji wa Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa Wamachinga, bodaboda, bajaji pamoja na wadau mbalimbali.

Aidha katika kikao kazi hicho Mheshimiwa Ludigija ametoa maelekezo kwa watendaji wote wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanasimamia vyema zoezi la ufanyaji biashara  kwani wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wameanza kurudi kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ambapo wanasababisha uchafu wa mazingira.

"Tumefanya kazi kubwa kuwapeleka wafanya biashara kwenye maeneo rasmi ambapo nia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni kuwawezesha wafanyabiashara wakiwa katika maeneo rasmi hivyo nielekeze wafanyabiashara wote ambao wamerudi kufanya biashara holela warudi kwenye maeneo yao rasmi tuliyowapanga Hivyo Wenyeviti wa Serikali za mitaa tuhakikishe mnatekeleza hili  ili tuweze kuendana na kauli mbiu ya 'Safisha, pendezesha, Dar es Salaam ili tuwe na sura nzuri ya Jiji la Dar es Salaam."

Sambamba na hilo Mheshimiwa Ludigija ameendelea kusema "Haiwezekani Mkuu wa Wilaya nifanye majukumu yangu na pia nifanye majukumu yako Mtendaji wa Kata hivyo naomba mhakikishe mnasimamia  na kutekeleza vyema majukumu yenu ya kazi."

Aidha Mheshimiwa Ludigija amewataka watu wa maegesho kuhakikisha wanakusanya ushuru wa  maegesho katika maeneo husika kwani ushuru wa maegesho umekua ni kero kwa Wananchi hivyo amewataka wakusanya ushuru wa maegesho wakusanye ushuru maeneo yao husika pia amewataka bodaboda wote, bajaji pamoja na watu wa maguta kupaki katika vituo tisa walivyopangiwa na sio kupaki holelaholea.

Akihitimisha kikao hicho Mheahimiwa Ludigija amesema "Niwaombe mfanye yote niliyowaelekeza na wenyeviti wa Mtaa tusaidiane kutekeleza kauli mbiu ya mkuu wa mkoa ya SAFISHA, PENDEZESHA DAR ES SALAAM hivyo niwakumbushe kuwa usafi wa mwisho wa mwezi huu utakaofanyika tarehe 30  utafanyika katika maeneo ya ‘Smart Area’  hivyo tujiandae kufanya usafi kwa  kuliweka Jiji letu safi.”

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.