• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Elimu zaidi yatolewa kuhusu lishe bora pamoja na usalama wa chakula

Tarehe iliyowekwa: August 31st, 2023

Maafisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi na mpangilio bora wa vyakula ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa yanayoweza kuwapata mara kwa mara.

Elimu hiyo imetolewa Leo tarehe 31 Agosti, 2023 katika siku ya Afya na Lishe kwa Kata ya Jangwani kwenye Mkutano uliowashirikisha Maafisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Viongozi wa Kata na Mitaa, Wananchi na wadau mbalimbali wa Afya pamoja Lishe.

Mbali na kufundisha kuhusu mpangilio bora wa mlo kamili somo lililofundishwa na Bi. Neema Mwakasege, wananchi pia walipata fursa ya kufundishwa namna ya kuandaa chakula cha mtoto mwenye umri wa kuanzia miezi sita na kuendelea ambapo Bi. Neema Manyama aliandaa uji wenye makundi matatu ya vyakula ambayo ni nafaka, maziwa pamoja na sukari.

Aidha, suala la lishe bora linakwenda sambamba na usafi pamoja na usalama wa chakula kuanzia shambani kinapotoka mpaka muda wa kuliwa. Bi. Safiona Mdee ambaye ni Afisa Lishe wa Kata ya Jangwani amesema kuwa ili chakula kiwe Safi na salama lazima taratibu na kanuni za usafi wa chakula zifuatwe.

"Ni vyema kuzingatia kanuni na taratibu za usafi na usalama wa vyakula hupita maeneo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa sio salama kabla ya kumfikia mlaji mfano sokoni ambapo uhifadhi wake unaweza kuwa si salama au shambani ambapo nafaka hupulizwa dawa za kuua wadudu ili zisiharibike haraka hivyo kufanya vyakula hivyo kuwa hatarishi kutumiwa moja kwa moja na mlaji bila kuchukua tahadhari yoyote." Amesema Bi. Mdee

Kwa upande wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wamewashukuru wataalamu kwa masomo mazuri waliyoyatoa kwao na kuwafanya wajifunze mambo mengi waliyokuwa hawayafahamu kuhusu lishe bora na kutoa wito kwa wananchi wa maeneo mengine kujitokeza kwa wingi pale Maafisa Lishe wanapowatembelea katika mitaa yao.    

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.