Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kipindi cha Robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 (Julai hadi Septemba 2023) ambapo leo tarehe 27 Oktoba, 2023 imetembelea miradi minne (4) ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Sekondari Kerezange, ujenzi wa majengo mapy matano katika Hospitali ya Wilaya Kivule, Ujenzi wa vyumba nae(8) vya madarasa Shule Mpya ya Sekondari Mvuti pamoja na ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Msingi Tungini.
Aidha, ujenzi wa Matundu ya vyoo Shule ya Sekondari Kerezange utekelezaji wa mradi uko hatua ya maandalizi na utagharimu shilingi milioni 40 pindi utakapokamilika , ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la Wodi 2 za wanaume na wanawake hospitali ya Wilaya Kivule uliogharimu shilingi milioni 200 ujenzi unaendeleaje huku ujenzi wa mfumo wa maji taka uliogharimu shilingi 100 ujenzi ukiwa umekamilika, katika ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Mvuti shilingi milioni 528.9 fedha kutoka mradi wa SEQUIP ujenzi uko kwenye hatua ya ukamilishaji wa miundombinu kwenye vyumba vya madarasa, jengo la Utawala, Maabara na Maktaba huku ujenzi vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Tungini uliogharimu shilingi milioni 40 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ujenzi umekamilika.
Akizungumza kwenye ziara hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala Mhe. Nyansika Getama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam fedha kwaajili ya ukamilishaji na uboreshaji wa miundombinu katika Hospitali ya Wilaya Kivule pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Mvuti ambazo zitarahisisha upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi wa maeneo ya mbali.
Naye, Mkuu wa Shule ya Msingi Tungini Mwl. Christopher Mwing'a ameeleza kuwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Msingi Tungini imesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi wakati wa kusoma huku akimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kutoa shilingi milioni 40 fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zilizokamilisha madarasa hayo na mpaka sasa wanafunzi wanasema bila msongamano wowote.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo imewataka Wahandisi wa Halmashauri wanaosimamia miradi kuhakikisha miradi inatekelezwa kulingana na makisio ya gharama za ujenzi (BoQ) inavyoelekeza lengo likiwa ni kufanya kazi kwa usanifu na umakini mkubwa, pia kamati imeagiza Wakandarasi kumaliza Miradi ndani ya muda uliopangwa na kwa usahihi huku ikitoa angalizo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na wataalamu wa ujenzi kuhakikisha wanatatua changamoto zilizojitokeza katika miradi hiyo kwani ubora wa miradi hiyo itasaidia idumu kwa muda mrefu na kuwapunguzia Wananchi wa maeneo ya jirani adha ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma hizo za kijamii.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.