Serikali ya Tanzania imedhamiria kuendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe nchini ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi imara kupitia maendeleo ya viwanda. “Maendeleo ya Taifa pamoja na mambo mengine, yanahitaji uwepo wa watu (nguvu kazi) wenye afya njema na lishe bora ili kuwawezesha kufanya kazi kwa bidii na Kuchochea maendeleo ya nchi."
Katika kutekeleza hilo leo Aprili 04, 2023 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia kitengo cha Afya na Lishe wameendelea kutoa elimu ya lishe kwa wananchi wa Kata ya Buguruni ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya lishe kwa watoto katika Kata 36 na Mitaa 159 ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya mwaka 2022/2023.
Aidha katika hafla hiyo wataalamu waliweza kupima hali ya lishe kwa watoto kuanzia miez 6 hadi miaka mitano lengo likiwa ni nikujua hali ya Afya ya watoto na kwa wale watakabainika kuadhirika na utapiamlo watapata rufaa ya kwenda kupata huduma katika kituo cha Afya anapoishi.
Akitoa mafunzo hayo ya lishe Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Neema Mwakasege amesema “Lishe bora ni kula chakula cha kutosha na chakula chenye virutubisho vyote muhimu. Lishe bora husaidia mwili kukua vyema, kuujenga mwili lakini pia huimarisha kinga ya mwili ili kuweza kupigana na magonjwa. Ili lishe iwe bora ni muhimu iwe na mchanganyiko wa Makundi sita ya chakula ambayo ni protini, wanga, fati, mbogamboga, madini, matunda na maji kwa wingi hivyo tuhakikishe tunawapa watoto mlo kamili lengo likiwa ni kupunguza udumavu na kuongeza uelewa kwa watoto wetu kwani lishe bora ndio msingi wa makuzi ya kimwili kwa watoto hawa.
Hata kama tunaanda mlo kamili tusipoandaa kwenye mazingira safi itakua ni kazi bure hivyo inabidi tuhakikishe tunaandaa vyakula hivyo katika mazingira, tunahifadhi chakula sehemu safi na salama pamoja na kuchemsha maji ya kunywa ili tukinge afya za watoto wasiadhiriwe na magonjwa nyemelezi”. Amesema Bi. Mwakasege
Sambamba na hilo Bi. Mwakasege amewahimiza wazazi/walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto kliniki hadi watakapofikisha miaka 5 ili kuweza kujua hali zao huku akiwataka wazazi/walezi ambao watoto wao hawajapata chanjo ya Surua wahakikishwe wanawapeleka kituo cha afya kupata chanjo hiyo ili wasije wakalemaa.
Kwa upande mwingine Afisa Ustawi kutoka Kituo cha Afya Buguruni Bi. Sophia Elias Kadonge amewataka wazazi/walezi kuhakikisha wanakata bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa ambayo inatumika kuanzia ngazi ya zahanati kituo cha afya mpaka hospitali za rufaa za Mkoa kama Hospitali ya Amana hivyo amewahimiza wazazi/walezi kukata bima ya afya iliyoboreshwa ili iweze kuwasaidia katika matibabu pindi mtu anapopata matatizo ya kiafya.
Sambamba na hilo Bi. Sophia Elias Kadoke amewataka wazazi/walezi kuwalinda watoto zidi ya ukatili wa kijinsia kwani janga hili linaonekana kuchukua nafasi kubwa sana katika Jamii zetu kwa sababu ya kukosa elimu ya namna ya kujikinga na matatizo haya hivyo amewaasa endapo mzazi/mlezi ataona dalili za ukatili au mtoto anafanyiwa ukatili ni vyema kutoa taarifa kwa maafisa ustawi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.