• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Tarehe iliyowekwa: June 5th, 2017

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameungana na Wananchi wengine ulimwenguni kote katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Maadhimisho haya katika ngazi ya Mkoa yamefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Siku ya Mazingira Duniani husheherekewa Ulimwenguni kote kila tarehe 5 Juni, kila mwaka. Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo Mazingira  na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira.

Awali, maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano kutokea viwanja vya Posta ya zamani hadi viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na mgeni rasmi Mhe. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul C. Makonda.

Mhe. Sophia Mjema baada ya kupokea maandamano na utambulisho wa viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa mazingira katika sekta binafsi na za umma alitoa shukrani za dhati kwa maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani na kupongeza juhudi za urejelezaji taka na kuwa mali zinazofanywa na wadau mbalimbali wa mazingira jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira jijini Dar es Salaam yalianza tangu tarehe 31 Mei, 2017 na kufikia kilele tarehe 5 Juni, 2017 ambapo shughuli mbalimbali zinazohamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali zikiwemo:

  • Upandaji wa miti 10,747 kulikofanywa na Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya wazi, maeneo ya mabondeni, mashuleni pamoja na maeneo ya pembezoni mwa barabara.
  • Usafi umefanyika kwenye maeneo ya mifereji, masoko na fukwe.

Mgeni rasmi aliendelea kueleza kwamba shughuli hizo ziliambatana na ukaguzi wa vifaa vya makampuni ya usafi na uhamasishaji kwa wananchi katika masula ya uhifadhi na usafishaji wa mazingira yanayowazunguka.

Mhe. Mjema ametoa wito kwa Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kufahamu kwamba wao wana wajibu wa kuzuia madhara na mabadiliko hasi katika Mazingira na kuwaasa watendaji na viongozi wa Serikali waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za kisekta na sheria ndogo za mazingira kuhamasisha jamii kufanya mazingira yao kuwa salama na masafi kwa lengo la ustawi wa maisha yetu na vizazi vyetu.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Sophia Mjema amewaomba wananchi wote wa Jiji la Dar es Salaam kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ili kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda, kuongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kuhimiza usafi wa mazingira na kuondoa utoroshaji wa raslimali katika nchi yetu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Sipora Liana pia alipata fursa ya kutembelea banda la vijana wajasiriamali wanaorejeleza taka ngumu na kuwa bidhaa mbalimbali na kuwaeleza mpango wa Halmashauri ya Jiji wa kujenga miundombinu ya viwanda vidogo vidogo ili kuweza kuwafikishia huduma muhimu  vijana na wanawake kwa pamoja ili wajikwamue kiuchumi, kujiongeza kipato na kupunguza tatizo la ajira hasa kwa vijana na kina mama kwa kuwarasimisha wajasiriamali hawa wadogo ambao wengi hawako rasmi kwa kukosa sehemu za kufanyia kazi.

Kauli mbiu inayoongoza maadhimisho haya kimataifa ni “Connecting People to Nature”. Kwa Kiswahili ni: “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira”. Kauli mbiu hii inahamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia yetu na kuhamasishana kuyatunza na kuhifadhi.

Pamoja na kauli mbiu ya kimataifa, kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira mwaka huu kitaifa ni "Hifadhi ya Mazingira: Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.” Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2017 katika ngazi ya Taifa yanafanyika kijijini Butiama Mkoani Mara, ambako Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alizaliwa, kukulia na kuzikwa. 

Madhumuni ya kupeleka maadhimisho haya Butiama ni kumuenzi Baba wa Taifa kwa sababu alikuwa mwanamazingira namba moja nchini mwetu lakini pia tunaenzi na kukumbuka mchango wake mkubwa katika masuala ya kuhifadhi mazingira nchini. Bila msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu hifadhi ya mazingira, bila falsafa yake kuhusu uhifadhi, na bila hatua madhubuti alizochukua kulinda mazingira ya asili ya nchi yetu mapema kabisa tulipopata uhuru, nchi yetu isingekuwa inasifika kwa uzuri wake na vivutio vyake.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.