Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji, Isaya Mwita leo tarehe 12 Machi, 2019 wamefanya Mkutano wa Baraza katika ukumbi wa Karimjee na kujadili taarifa za utendaji kazi wa kila siku na za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Oktoba-Desemba).
Wakazi na wadau mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki Mkutano huo na kusikiliza mawasilisho ya taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwa Wenyeviti wa Kamati za Fedha na Uongozi, Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Mipango na Uratibu na Kamati ya Maadili.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.