Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto amewataka Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanatekeleza dhima ya Sera na Utawala bora kama ilivyo katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Hayo ameeleza leo Juni 22, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mnyamani.
Akiongea katika hafla hiyo Mhe. Kumbilamoto amempongeza Diwani wa Kata ya Mnyamani kwa juhudi alizozionesha hadi kujengwa kwa ofisi hiyo kwani awali wananchi walikua wanapata changamoto za kupata huduma, hivyo baada ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya Kata wananchi wa Kata hii watapata huduma kwa ukaribu na haraka zaidi.
“Nimpongeze Diwani wa Kata ya Mnyamani Mhe. Shukuru Dege kwa kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa ukaribu. Ofisi hii imegharimu takribani shilingi Milioni 130 ikiwa na vyumba 9 pamoja na ukumbi wa mikutano ambao utasaidia katika shughuli zote za Kata.”
Sambamba na hilo Mhe. Kumbilamoto ametoa wito kwa Madiwani wengine wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaainisha miradi yote iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuhakikisha miradi hiyo inafuatiliwa kwa ukaribu zaidi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.