Waheshimiwa Madiwani na wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles leo tarehe 27 Mei, 2019 wamekutana katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya Mkutano wa Baraza wa robo ya tatu ya mwaka kwa kipindi cha Januari hadi Machi, kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mkutano huo wa Baraza pia umehudhuriwa na wananchi mbalimbali Jiji la Dar es Salaam ambao wamepata fursa ya kusikiliza mawasilisho ya taarifa za kila siku na za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwa wawakilishi wao ambao ni Wenyekiti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.