Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Ndg. Amour Hamad Amour leo tarehe 29 Mei, 2017 amezindua Mradi wa Maboresho ya Mtaa wa Samora Jijini Dar es Salaam katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Japan kupitia JICA ambao unagharimu jumla ya Dola za Kimarekani 400,000 na ulianza kutekelezwa mnamo mwezi Januari, 2017 na unatarajiwa kukamilika mnamo mwezi Julai, 2017.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya mifano ambayo imeandaliwa kwa pamoja na wataalam wa JICA na wa Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania zinazojihusisha na usafiri/usafirshaji katika Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.