Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Juni 25, 2024 ameshiriki mkutano wa Baraza la Madiwani la Jiji la DSM la kupokea hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) za mwaka 2022/2023.katika ukumbi wa Arnatoglou.
RC Chalamila akiongea katika Baraza ilo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa na historia ya kupata hati safi kwa kipindi cha miaka 8 mfululizo ambapo amewataka kuendeleza utamaduni huo na namna pekee ya kuendeleza utamaduni huo ni kuzingatia maagizo na maelekezo ya CAG pamoja na kuzingatia ushauri unatolewa na wakaguzi wa ndani (Inernal Auditors)
Aidha, RC Chalamila amepongeza umahiri wa Halmashauri ya Jiji katika ufungaji wa hoja za CAG ambapo takribani 62% ya hoja zimefungwa hivyo amewataka kuhakikisha wanamalizia kufunga hoja chache zilizobakia.
Sambamba na hilo, RC Chalamila ameridhishwa na kufurahishwa na kasi ya ukusanyaji kodi katika jiji hilo ambapo hadi sasa makusanyo yako zaidi ya 108% rai yake kwa Halmashauri hiyo kujipanga zaidi kubuni na kusimamia vema vyanzo vya mapato lakini pia kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile vituo vya kisasa vya Afya na masoko kwa kutumia fedha za ndani.
Vilevile, Baraza hilo lilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Toba Nguvila, viongozi wa chama, wataalam kutoka Ofisi ya Mkoa wa DSM na wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Awali akiongea katika hafla hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa nasaa zake na kuahidi kwa niaba ya waheshimiwa madiwani kufanyia kazi maagizo yake kwa masilahi mapana ya wana Ilala, Mkoa na Taifa kwa Ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.