Na:Amanzi kimonjo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla leo September 1, 2021 amefanya ziara maalumu inayolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Jimbo la Segerea ambapo mamia ya wananchi wa Jimbo la Segerea wamejitokeza katika viwanja nya Buguruni Ghana ili kuweza kuwasilisha kero zao.
Aidha miongoni mwa kero zilizoweza kuwasilishwa na Wananchi wa Jimbo la Segerea kwa Mkuu wa Mkoa Mh. Makala ni Pamoja na migogoro ya ardhi, ufanyaji biashara holela, kero ya Mitaro, ubovu wa miundombinu ikiwepo ubovu wa barabara, sekta ya Afya, sekta ya Maji na uchafu wa mazingira
Katika Mkutano huo RC. Makala ameweza kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Segerea ikiwemo kero za ardhi ambapo imeonekana wananchi wengi wanakabiliwa na kero ya migogoro ya ardhi ikiwemo migogoro ya viwanja na maeneo wanayoyamiliki kumilikiwa na watu wengine, pia kwa baadhi ya kero RC. Makalla aliweza kuzielekeza kwa Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanafuatilia kero hizo ili kuweza kuzitatua na kuzipatia ufumbuzi.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesisitiza Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kushiriki kuchoma chanjo ya UVICO 19.”wajibu wetu ni kuhamasisha kuhusu chanjo, fanya maaamuzi Raisi amechanja, mimi nimechanja na wewe fanya maamuzi ya kuchanja kwani mabanda katika Viwanja vya Buguruni Ghana yapo na chanjo hivyo tujitokeze kwa wingi kuchanja siku hii ya leo ambapo chanjo imetufikia mahali tulipo kwani Mkoa wa Dar es Salaam umeshika nafasi ya kwanza kitakwimu kuwa na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuchoma chanjo ya UVIKO – 19.”Amesema RC. Makalla
Sambamba na hilo mabanda hayo pia yameweza kutufikishia huduma nyingine za afya kama kupima malaria, sukari, presha Pamoja na UKIMWI kwani huduma hizo zinatolewa bure bila malipo yeyote.
Katika Mkutano huo RC. Makala amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Segerea ikiwemo kero za ardhi ambapo imeonekana wananchi wengi wanakabiliwa na kero ya migogoro ya ardhi ikiwemo migogoro ya viwanja na maeneo wanayoyamiliki kumilikiwa na watu wengine, pia kwa baadhi ya kero RC. Makalla aliweza kuzielekeza kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanafuatilia kero hizo ili kuweza kuzitatua na kuzipatia ufumbuzi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.