Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo tarehe 25 Septemba, 2019 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Halmashauri ya Jiji ikiwemo Mradi wa ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani katika eneo la Mbezi Luis.
Akizungumza katika kikao maalum kilichowakutanisha, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakandarasi, Washauri wa Miradi na Viongozi wa sekta mbalimbali, Makonda amewataka viongozi hao kutoa taarifa katika ofisi husika kuhusiana na changamoto za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mradi wa ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani katika eneo la Mbezi Luis unagharimu kiasi cha Sh. 50.09 bilioni fedha za Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya kimkakati.
Utekelezaji wa mradi huu ulianza kwa kulipa wananchi fidia ya takribani Sh. 7.8 bilioni zilizolipwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mradi utakapokamilika unatarajia kuiingizia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wastani wa Sh. Bilioni 7.2 kwa mwaka. Ujenzi wa Kituo hicho utakamilika mwezi Julai, 2020. Kwa sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 35.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.