Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo tarehe 24 aprili, 2019 ametembelea kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi mkakati wa ujenzi wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani wa Mbezi Luis na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho.
Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa RC Makonda, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana alieleza ujenzi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis ni mradi unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya kimkakati na hadi kufikia Machi mwaka huu ulikua umekamilika kwa asilimia 12.5.
Akiwa katika mradi huo Makonda amehimiza kuzingatia ushirikishwaji wa wazawa katika mradi huo mkubwa ili waweze kunufaika zaidi na hata malighafi zinazotumika katika ujenzi zitumike zile zinazozalishwa nchini ili kuongeza kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.