• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Shilingi Bilioni 10.75 kutekeleza Miradi ya Ujenzi wa Barabara Jiji la DSM

Tarehe iliyowekwa: July 15th, 2024

Shilingi bilioni 10.75 fedha kutoka mapato ya Halmashauri zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa barabara Jiji la Dar es Salaam  kwa kiwango cha lami na zege. Hayo yamebainishwa leo Julai 15, 2024 na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomaary Satura kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara 10 kati ya Jiji la Dar es Salaam na wakandarasi wanaoenda kutekeleza miradi hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Wakandarasi kuwa waadilifu kwa kuhakikisha wanakamilisha miradi kwa wakati huku akiwasisitiza washirikiane katika kazi ili kuleta matokeo yenye tija kwa maslahi ya Wananchi.

Sambamba na hilo Mhe. Mpogolo ametoa pongezi kwa Mstahiki Meya na Madiwani kwa usimamizi mzuri wa miradi huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Watendaji wa Jiji kwa kasi ya ukusanyaji wa mapato ambao umekua chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazotoa kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku akitoa wito kwa Wakandarasi kutekeleza miradi kwa wakati uliopangwa ilo waweze kutimiza adhma ya Rais ya kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Jomaary Satura ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imejipanga kuboresha ustawi wa maisha ya wananchi kwa kuzingatia nyanja zote muhimu ikiwemo elimu, afya na miundombinu hivyo katika kutekeleza hilo JiJi la Dar es Salaam limeweza kutenga asilimia 10 za mapato ya ndani kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambapo bilioni 10.7 itatumika kutekeleza miradi hiyo.

“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tumekusanya shilingi bilioni 111 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 sawa na ongezeko la bilioni 30 ikilinganishwa na mwaka 2022/2023 hivyo kutokana na mapato haya kuongezeka, shilingi bilioni 10.7 imetengwa kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara 10 za ndani Jiji la Dar es Salaam zinazoenda kutekelezwa kwa kiwango cha lami na zege na leo tunasaini mikataba na wakandarasi wanaoenda kutekeleza miradi hiyo, hivyo niimani yangu wakandarasi waliochaguliwa ni wakandarasi wenye uwezo wa kujisimamia wenyewe na watakamilisha mradi kwa wakati pia niwatake muwe waadilifu kwa kutekeleza majukumu ipasavyo kwa faida ya watanzania wengine.” Amesisitiza Ndg. Satura.

Naye Mkandarasi kutoka Kampuni ya Southern Link Bw. John Mosha ameishukuru Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuchaguwa wakandarasi wazawa huku akiwahakikishia kutekeleza miradi hiyo kwa kiwango bora na kwa wakati.

Aidha, Miradi hii inatarajiwa kukamilika ndani ya muda wa miezi mitatu.


















Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.