• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) laahidi kushirikiana na Tanzania katika kuboresha Sekta ya Elimu

Tarehe iliyowekwa: December 1st, 2023

Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) laahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu Nchini, hayo yamebainishwa leo Desemba Mosi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa GPE, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bi. Laura Frigenti wakati wa ziara yao ya kutembelea shule ya Msingi Mikongeni iliyoko Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kukagua miradi ambayo GPE imechangia kwenye shule hiyo.

Akiongea wakati wa ziara hiyo Dkt. Kikwete ameeleza kuwa “Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani ni wadau wetu muhimu sana kwenye kuhakikisha sekta ya elimu inakua kwa kasi nchi kwani kupitia shirika hili toka mwaka 2013 tulipoingia makubaliano nao Serikali ya Tanzania tumeweza kupokea Dola milioni 332 kwaajili ya kuendeleza sekta ya elimu, kuchapisha na kusambaza vitabu vya kiada milioni 10 Shuleni, hata hivyo tayari GPE imetia saini na Serikali, makubaliano ya kutoa dola milioni 80 (zaidi ya shilingi Bilioni 201) kwaajili ya kusaidia mafunzo ya walimu nchini hivyo nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ushirikiano huu pamoja na kuridhia kikao kifanyike nchini Tanzania ambapo Mimi kama Mwenyekiti wa GPE nitaongoza vikao vya Bodi vya Shirika hilo huko Zanzibar tarehe 4 hadi 6 Disemba ikiwa ni mara ya kwanza kwa Shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika.”

Sambamba na hilo Dkt. Kikwete ameendelea kusema GPE itaendelea kusimama na Tanzania ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inaendelea kukua kwa kasi pamoja na kuhakikisha haki kwa kila mwanafunzi huku akisisitiza fedha zinazotolewa na GPE kwaajili ya kuboresha miundombinu ya elimu zitumike kama inavyotakiwa.

Kwa upande wake  Afisa Mtendaji Mkuu  wa GPE Bi. Laura Frigenti ameeleza kuwa wao kama GPE wanafuraha  kubwa kuja Tanzania kukagua miradi yao huku akisisitiza kuwa ushirikiano wa GPE na Tanzania ni wa muda mrefu na utasaidia watoto wadogo kupata elimu kwaajili ya kutimiza ndoto zao.

Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb) amesema kuwa “Nipende kutoa shukrani zangu kwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na GPE wote kwa ujumla kwa kutembelea Tanzania kujionea miradi yenu na jitihada mnazozionesha kuhakikisha sekta ya elimu nchini inakua kwa kasi.”

Awali akitoa taarifa kwa wageni hao Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mikongeni Mwl. Saimon Mndendemi ameeleza kuwa kupitia shirika la GPE shule imepokea shilingi milioni 55. 8 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya awali pamoja na matundu 6 ya vyoo ambayo yameweza kuwa mchango mkubwa kwa shule kwani wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na rafiki, pia ameshukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi huo shule ya mikongeni hivyo wanaahidi kuyatunza madarasa hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.

Ikimbukwe kuwa GPE ni Shirika lililolenga kusaidia nchi zinazoendelea ili watoto waweze  kupata elimu bora huku wakitoa kipaumbele kwenye elimu ya mtoto wa kike ambapo katika nchi 180 za GPE Tanzania ikiwa mojawapo.




Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.