Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wameadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kutoa msaada wa vifaa 40 vya kuhifadhi taka kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 07 Oktoba, 2017.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Zanzibar, Vicky Bishubo amesema msaada huo wa vifaa vya kuhifadhi taka umetokana na mchango wa fedha kutoka kwa Wafanyakazi wa matawi yote ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
“Tunakabidhi vifaa vya kuhifadhi taka 40 kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4 kwa lengo kuchangia juhudi za udhibiti na uhifadhi taka ngumu zinazozalishwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ili kuliweka Jiji katika mazingira safi na salama,” alisema Bishubo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora J. Liana aliwashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam kwa msaada ambao wameutoa na kuchangia juhudi za udhibiti na uhifadhi wa taka ngumu zinazozalishwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
Aidha Mkurugenzi wa Jiji amewaomba wafanyakazi hao wa Benki ya NMB kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.