• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Wajumbe TSC wahimizwa kusimamia Utumishi na Maadili ya Walimu

Tarehe iliyowekwa: September 25th, 2024

Wajumbe wa Kamati za Nidhamu za Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC) kwa ngazi ya Wilaya wamehimizwa kuendelea kutekeleza jukumu la Msingi la kuhakikisha wanasimami Utumishi na Maadili ya Walimu ili kuwa na Walimu wenye kujituma na wanaozingatia maadili ya kazi yao kwaajili ya kuwalea watoto kwa usahihi na kuboresha elimu nchini.

Wito huo umetolewa leo Septemba 25, 2024 na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Zainab Katimba (Mb) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya wajumbe wa Kamati za nidhamu za Tume ngazi ya Wilaya yanayofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki iliyojumuisha Wilaya za Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro.

Akiongea wakati wa ufunguzi huo, Mhe. Katimba ameipongeza Tume ya Utumishi wa Walimu pamoja na wajumbe wake kwa utendaji mzuri wa kazi unaoambatana na uzoefu na uaminifu katika kutekeleza Majukumu yao.

"Nipende kutoa pongezi zangu kwa Tume pamoja na wajumbe wa Kamati kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuhakikisha mnateleleza majukumu ya kisheria pamoja na kusimamia utumishi wa Walimu kwani mafunzo haya yana lengo la kuwawezesha wajumbe wa Kamati kufahamu wajibu wao katika kusimamia ajira, nidhamu na maadili ya Walimu hivyo ni imani yangu mafunzo haya yatakua chachu ya kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Tume na Serikali kwa Ujumla lengo likiwa ni kuendana na kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhun Hassan ya 'Kazi Iendelee' na Sisi kama viongozi tutaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kazi ziendelee kufanyika kwa ufanisi na uadilifu." Amesisitiza Mhe. Katimba.

Awali akitoa salamu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Prof. Masoud Mureke ameeleza kuwa lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo wenyeviti na wajumbe wa Kamati za Tume za Wilaya ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku akiahidi kuwa Tume itaendelea kusimamia jukumu lake la msingi la usimamizi wa Utumishi na Maadili ya Walimu kwa lengo la kuhakikisha Walimu hao wanazingatia maadili kwa manuafaa ya watoto na kuendelea kuboresha Elimu Nchini.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi wa Tume Wilaya ya Ilala Mwl. Subira Mwakibete ameeleza kuwa baada ya mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengee uwezo wajumbe wa Kamati za Tume za Wilaya ni imani kwao wataendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuhakikisha sekta ya elimu nchini inakua na Walimu wanatimiziwa stahiki zao muhimu kwa wakati.

Aidha, Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku Siku mbili (2) kwa wajumbe wa wilaya 139 kwa Kanda tano (5) ambazo ni Kanda ya Kaskazini ambapo mafunzo yanafanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Jiji la Arusha kwa Wajumbe wa Wilaya za Mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, Kanda ya Mashariki ambapo mafunzo yanafanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kwa Wajumbe wa Wilaya za Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, Kanda ya Kati ambapo mafunzo yanafanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika Manispaa ya Tabora kwa  Wajumbe wa Wilaya za Mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora, Singida, Tabora na Dodoma, Kanda ya Ziwa ambapo mafunzo yanafanyika katika Ukumbi wa Nyakahoga Jijini Mwanza   kwa Wajumbe wa Wilaya za Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita pamoja na Kanda ya  Nyanda za Juu Kusini ambapo mafunzo yanafanyika katika Ukimbi wa Dkt. Shein Jijini Mbeya kwa Wajumbe wa Wilaya za  Mikoa ya Rukwa, Songwe, Ruvuma, Njombe, Iringa na Mbeya.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.