Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam kupitia Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii imetoa elimu juu ya kuzingatia lishe kwa kina mama wajawazito katika Zahanati ya Vingunguti.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Lishe wa Jiji la DSM Bi. Neema Mwakasege amesema kuwa lishe ni muhimu kwa kina mama hasa wajawazito sababu wanapokua katika hali hii wanahitaji madini mengi mwilini hivyo ni muhimu kuzingatia.
Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Vingunguti Dkt. Isaack Makundi amesema anashukuru kwa elimu hiyo endelevu kutoka Jiji la Dar Es Salaam kupitia Jiko Darasa kwa wajawazito na kuwashukuru waliojiotokeza na na kusisitiza kuzingatia yale wanayoelekezwa na wataalamu.
Ikumbukwe kuwa ajenda hii ya lishe ni moja kati ya mipango endelevu ndani ya Jiji la Dar Es Salaam na Taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kila mwananchi kuzingatia lishe bora kwa Ustawi wa Jamii.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.