Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Mei 15, kupitia Idara ya Afya chini ya Ofisi ya Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI imeendesha zoezi la Upimaji wa Afya kwa hiari mahali pa kazi kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa upimaji, mratibu wa zoezi hilo Anna Kagya amesema "Zoezi limekua na Muitikio mkubwa, watumishi wengi wamejitokeza kufanya vipimo na hii imesaidia sana kwakua huduma imesogezwa karibu yao na hatutaishia hapa baada ya watumishi huduma hizi tunazipeleka mitaani kwa wananchi."
Moja kati ya watumishi waliojitokeza ndugu Mosi Mgaza ameeleza kufurahishwa na kusogezewa huduma hizo kazini na kwamba imemsaidia kutambua hali ya afya yake "Nimehamasika kupima sukari kwakua kila siku tunapewa tahadhari kwamba vifo vya magonjwa yasiyoambukiza vinaongezeka kila siku kwahiyo majibu ya vipimo hivi yananisaidia kuendelea kujiweka sawa. "
Miongoni mwa huduma zilizotolewa katika zoezi hilo ni pamoja na upimaji wa Shinikizo la Damu, Uzito, Kisukari, VVU, Elimu ya lishe pamoja na ushauri nasihi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.