JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Mradi wa Redio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inayopatikana katika masafa ya 91.7 Mhz FM Band unamilikiwa na Halmashauri ya Jiji kwa asilimia 100. Mradi huu ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2010/2011 kwa kuanza na ukarabati wa studio za redio zinazopatikana katika majengo ya Halmashauri Makao Makuu (City Hall) kona ya mitaa ya Edward Moringe Sokoine na barabara ya Morogoro. 

Matangazo ya majaribio yalianza kurushwa tarehe 11 Septemba, 2013. Leseni ya Utangazaji (Radio Communication Station Licence) ilitolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) tarehe 9 Mei, 2014.  


MALENGO YA MRADI 

Halmashauri ya Jiji iliazimia kwamba hadi kufikia mwaka 2017 iwe imefanikiwa kuanzisha kituo cha redio  ikiwa na malengo yafuatayo:

       (i)   Kutangaza mafanikio ya Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Jiji la Dar es Salaam.

      (ii)   Kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi, kuwaelimisha na kutoa burudani kupitia vipindi vya redio hiyo.

     (iii)  Kutoa ajira hususan kwa vijana.

     (iv)  Kuongeza vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Jiji.