JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Utangulizi

Jiji la Dar es Salaam lipo kati ya latitudo nyuzi 6 hadi 7 na longitudo kati 39.45 kwa upande wa Mashariki na nyuzi 39 kwa upande wa magharibi, Kusini mwa ikweta na upande wa magharibi, Kusini na Kaskazini. Jiji linapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki linapakana na Bahari ya Hindi. Jiji la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi. Jiji hupata joto la wastani wa kati ya nyuzi 25 hadi 33 na mvua katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba – Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi – Mei.

 

Idadi ya watu

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Jiji lina idadi ya watu 4,364,541, ambapo kati yao wanaume ni 2,125,786 na wanawake ni 2,238,755.

 

Historia ya Halmashauri ya Jiji

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)

Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.

Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la Serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.

Tume ya Jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sheria na. 6 ya mwaka 1999.


Utawala

Kiutawala Jiji limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:


Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Jiji ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa. Jiji inaongozwa na BARAZA LA MADIWANI lenye wajumbe 31


Muundo wa Jiji

Halmashauri ya Jiji ina majukumu yake tofauti na yale ya Halmashauri za Manispaa, Halmashauri za Manispaa zina uongozi unaojumuisha Meya na Madiwani ambao huchaguliwa na wananchi kidemokrasia. Aidha Mkurugenzi wa Manispaa huteuliwa na Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa.

Halmashauri ya Jiji inaundwa pia na Wabunge wenye Majimbo ya uchaguzi na Viti Maalum Mkoani Dar es Salaam pamoja na Mameya na Madiwani watatu kutoka kila Halmashauri za Manispaa.

Wajumbe hao huunda Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji chini ya uongozi wa Meya wa Jiji ambaye huchaguliwa na Madiwani wote wa Mkoa wa Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Jiji ambaye huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni Mtendaji Mkuu wa Halmashauri na Katibu wa Baraza la Madiwani.Majukumu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliundwa na kupewa majukumu ya kuratibu na kusimamia shughuli za uendelezaji wa Jiji katika Halmashauri za Manispaa zote tatu. Majukumu hayo ni kwa mujibu wa Sheria za serikali za mitaa (Mamlaka za Miji) Na.8 ya mwaka 1982 kifumgu cha 69A kama ilivyorekebishwa na sheria na.6 ya mwaka 1999.

Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:

Uboreshaji wa Muundo wa Jiji la Dar es Salaam kuwa mamlaka sita umeleta ufanisi mkubwa katika utoaji bora wa huduma kwa jamii kwani madaraka yamesogezwa karibu zaidi na wananchi.