JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Programu ya kuboresha na kuendeleza miundombinu mitaani ni program inayotekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa miundombinu na huduma katika maeneo yasiyopangwa ya Jiji.

Kwa kulitambua tatizo la kutopangwa eneo kubwa la Jiji, Serikali kuu pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamefanya jitihada ili kuweza kukabiliana na tatizo hili.

Programu ya kuboresha miundombinu mitaani ilianza rasmi mwaka 2001 na ilitarajiwa kuzifikia kata 9 kati ya 56 ya maeneo ya makazi yasiyopimwa Jijini Dar es Salaam. Programu hii itatekelezwa kwa awamu mbili takribani zenye ukubwa sawa.

Katika awamu ya kwanza ya program, kaya zitakazonufaika na uboreshaji wa miundombinu zitachaguliwa kulingana na mchakato endelevu wa ushauriano ambao utahusisha kutambua matatizo, vipaumbele vya kukabiliana navyo na jinsi gani ya kukabiliana na changamoto tajwa.

Awamu ya pili ya program hii itahusisha kaya ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa katika uboreshaji wa miundombinu.

Kaya 31 zinatarajiwa kunufaika na programu ya kuboresha miundombinu mitaani. Kaya hizi 31 zitanufaika na program hii na zinaunda wastani wa watu 330,000.

Program ya kuboresha miundombinu ya makazi mitaani inatarajiwa kufikia eneo la hekta 1000 au takriban 20% ya eneo lisilopangwa la Jiji na inatarajiwa kuboresha miundombinu inayohusisha huduma zifuatazo:


 Hatimaye kaya 31 zitanufaika kwa pamoja na programu ya usambazaji maji na uboreshaji wa miundombinu yake unaofadhiliwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam. Mradi ambao utaweka mabomba ya maji ya umma na kuunganisha kila nyumba.