JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam zinatarajia kuanzisha eneo maalum la usafi wa mazingira (Smart Area) ikiwa ni sehemu ya juhudi za mamlaka hizo za kuliweka Jiji katika mazingira safi, kuwezesha wananchi kushiriki kimilifu katika shughuli za usafi na kutunza mazingira yao kama suluhisho la kudumu la kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na daima kuliweka Jiji safi.

Katika utekelezaji wa mpango huo utakaoratibiwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Temeke na Ilala wananchi watapaswa kushiriki kikamilifu kwa kutambua, kuzingatia na kukubali kwamba:

 

Katika utekelezaji wa mpango huo, maeneo yafuatayo yamepangwa kuwa Smart Area wakati maeneo mengine yataendelea kuwa chini ya usimamizi wa karibu wa Halmashauri za Manispaa katika kuimarisha usafi wa mazingira:

· Barabara ya Kawawa: kuanzia makutano ya Barabara ya Kawawa na Uhuru hadi makutano ya Barabara ya Kawawa na Ali Hassan Mwinyi (Morocco)

· Barabara ya Ali Hassani Mwinyi: kuanzia makutano ya Morocco hadi Salenda Bridge, maeneo ya fukwe na makutano ya Barabara Kilwa na Mandela (Uhasibu), kuelekea makutano ya Barabara ya Nyerere na Mandela (Tazara)

· Barabara ya Nyerere: kuanzia makutano barabara ya Nyerere na Mandela (Tazara) hadi makutano ya Barabara ya Kawawa na Uhuru.

· Maeneo ya vivutio vya watalii hususan fukwe

· Barabara zinazotumika kwa ajili ya mapokezi ya wageni (hususan viongozi) wa nje ya nchi: Barabara ya Nyerere kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Barabara ya Mwai Kibaki hadi Hoteli ya Whitesands kupitia Barabara ya Mbezi Chini.

· Barabara ya Morogoro na Barabara zote za Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transit(DART)

 

Madhumuni ya mpango huo ni kuwa na usimamizi madhubuti wa sheria, kanuni na taratibu za uendashaji miji ili kuliondoa Jiji katika changamoto za muda mrefu zinazosababishwa na uchafu. Jambo la msingi zaidi ni kwamba eneo hili litawekwa miundombinu madhubuti itakayorahisisha utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kutokomeza magonjwa ya mlipuko yanayoathiri maisha na maendeleo ya wakazi wa Dar es Salaam.