JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

1. Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu

Ni miongoni mwa Vitengo vinne vilivyoko chini ya Ofisi ya Mkurugenzi katika Muundo wa Halmashauri ya Jiji ulioidhinishwa mwaka 2005 na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Pamoja na jukumu la kuratibu shughuli za maendeleo ya Halmashauri ya Jiji, Kitengo hiki kina majukumu makubwa yafuatayo:

2. Kitengo cha Ugavi na Manunuzi

Kitengo cha Ugavi ni moja wapo ya Vitengo vilivyo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi katika Halmashauri ya Jiji. Kazi kubwa ya Kitengo ni kuhakikisha inatekeleza Sheria  mpya ya Manunuzi Na. 7 ya mwaka 2011, na Kanuni ya Manunuzi Na. 446 ya mwaka 2013 na kuhakikisha kuwa manunuzi hayo yanafuata na kuzingatia Sheria na Kanuni hizo. Vile vile Kitengo kinatoa ushauri kwa Idara na Vitengo kufuata Mpango wa Manunuzi.  

3. Kitengo cha TEHAMA, Itifaki na Uhusiano 

Kitengo hiki kina majukumu ya kusimamia utekelezaji wa kazi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), City FM Radio na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Halmashauri ya Jiji kwa vyombo vya habari. Majukumu mengine ni kufanya mawasiliano na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, kuendeleza uhusiano baina ya Halmashauri ya Jiji na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Uhusiano wa Miji Dada.