Shirika la maendeleo na uchumi la Jiji la Dar es Salaam ni Shirika la umma lililoanzishwa na serikali mnamo tarehe 18/05/1971. Shirika liliundwa chini ya sheria ya makampuni namba 212 ya mwaka 1971 mpaka 1973 lililopowekwa chini ya sheria namba 16 ya mashirika ya maendeleo ya Wilaya(District Development Cooperation Act no 16).
Shirika la DDC lilianzishwa kama kitega uchumi cha Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam kwa lengo la kufanya shughuli za uzalishaji, biashara na burudani kwa ajili ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Dira ya Shirika la DDC ni kuwa taasisi inyoongoza kiuchumi ndani ya ushindani kwa kutoa huduma yenye tija na za kudumu ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
Dhamira ya Shirika la DDC ni kutoa huduma kwa watu wa Dar es Salaam yenye ubora wa hali ya juu kwa wateja kwa kuendeleza masoko ya kisasa kulingana na mabadliko ya mazingira ya sasa.
Dhumuni kuu la Shirika la DDC ni kufanya biashara yoyote halali yenye kuleta faida kwa Shirika ikiwa ni pamoja na biashara za jumla na rejareja
NB:Shirika hutekeleza majukumu haya kwa kukodisha na kushirikisha taasisi binafsi na za umma
Shirika la DDC linaongozwa na wajumbe saba(7) na wanaoteuliwa na Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Shughuli za shirika zinasimamiwa na kutekelezwa na menejimenti ya watu watano(5) akiwemo Meneja Mkuu na Wakuu wa Idara wanne(4); Idara ya Utumishi na Utawala, Ugavi, Fedha na Mipango na uwekezaji. Kazi kubwa ya watendaji ni kusimamia rasilimali watu, shughuli za miradi pamoja na mapato na matumizi ya Shirika.
Shirika lina miradi saba(7). Miradi hiyo ni:-
(i) DDC Kariakoo
Mradi huu una ghorofa tatu, vibanda vya maduka, ofisi, migahawa na baa ambavyo vinakodishwa kwa watu na taasisi binafsi kwenye jengo hili ndipo yalipo Makao Makuu ya Shirika.
(ii) DDC Mlimani
Katika mradi huu shughuli kuu ni baa na majiko, vibanda vya biashara na ofisi ambavyo vimekodishwa kwa watu binafsi
(iii) Perval Garage
Mradi huu ni wa ghorofa moja na bohari mbili ambao upo eneo la banda la ngozi Barabara ya Nyerere. Majengo yote yamepangishwa kwa mpangaji mmoja aitwaye JAMBO FREIGTH anayefanya biashara ya usafirishaji wa mizigo.
(iv) DDC Keko
Mradi huu upo kwenye ukarabati wa kumbi za burudani, kwa sasa vibanda vya biashara na ofisi pekee ndivyo vinafanya kazi .
(v) DDC Magomeni
Mradi huu upo sehemu maarufu kwa shughuli za burudani na muziki jijini Dar es Salaam eneo la Magomeni Barabara ya Kondoa kwa sasa mradi upo kwenye uwekezaji na shughuli kuu zinazolengwa ni kumbi za burudani, baa, migahawa, ofisi na vibanda vya biashara.
(vi) Shamba la Malolo
Shamba hili lina ukubwa wa hekari 5,000 lipo eneo la Mabwepande Manispaa Kinondoni na Ubungo jijini Dar es Salaam. Shirika limebadilisha matumizi ya shamba hili na kulenga kufanya eneo la viwanda vidogodogo na kutengeneza miji ya kisasa (Satellite Town) na kupima viwanja vya makazi.
(vii) Shamba la Ruvu
Shamba hili lenye ukubwa wa hekari 10000 lipo mkoa wa Pwani kijiji cha Magindu. Mradi huu ni kwa ajili ya kunenepesha mifugo na kutoa huduma kwa wafugaji. Kwenye mradi huu kuna mabwawa makubwa ya kunyweshea mifugo na Shirika limetengeneza majosho ya kuoshea wanyama.
Shirika lina mikakati ya kuboresha huduma zake na kuwa zenye tija zaidi kwa kuwekeza katika maeneo yafuatayo:-
(i) Uwekezaji DDC Magomeni
Shirika linamiliki eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zipatazo 6013 katika Barabara ya Kondoa Magomeni maarufu kama DDC Magomeni. Shirika lipo katika mchakato wa kujenga jengo la ghorofa tisa (9) lenye matumizi mbalimbali ya vibanda vya biashara, mabenki, ofisi, kumbi za mikutano na sherehe/ burudani. Shirika linakaribisha taasisi binafsi na za umma tuwekeze kwa ubia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
(ii) Uwekezaji DDC Keko
Shirika lina mpango wa kuboresha huduma za burudani kwenye mradi huu kwa kujenga kumbi za bati na kukarabati vyumba vya maduka yaliyopo eneo hili maarufu kwenye utoaji wa burudani, biashara na bohari pembezoni ya barabara ya Chang’ambe Keko. Hapo baadae Shirika litajenga jengo la ghorofa zaidi ya tano kwa ajili ya bohari, gereji, kumbi za burudani, baa, migahawa, ofisi za makampuni na vyumba vya biashara.
(iii) Uwekezaji Kariakoo DDC
Shirika la DDC lina eneo la DDC Kariakoo lenye ukubwa la mita la mraba 2500. Shirika lina mpango wa kujenga jengo la kisasa lisilo pungua ghorofa kumi ili kufanya biashara mbalimbali; ikiwemo vibanda vya maduka, migahawa, benki, kumbi mbalimbali, supermakerts, bureau de change, ofisi n.k. Shirika linakaribisha taasisi binafsi na za umma kuwekeza kwa pamoja katika eneo hili lenye mvuto wa kibiashara zaidi jijini Dare s Salaam na Tanzania.
(iv) Uwekazaji DDC Mlimani
Shirika lina mpango wa kujenga jengo la ghorofa zipatazo kumi kwenye eneo hili lenye mvuto mkubwa wa kibiashara na kihistoria ya burudani mkabala na Mlimani City Barabara ya Chuo Kikuu, Makongo. Kutakuwa na maduka zaidi ya 200, kumbi za burudani kubwa na za kati kwa ajili ya muziki, sherehe na mikutano, ofisi za makampuni na watu binafsi, baa na migahawa na maegesho.
(v) Uwekezaji DDC Mlimani Mlalakuwa
Shirika linampango wa kujenga jengo la ghorofa tano la kitega uchumi cha hosteli. Jengo hili litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wapatao elfu tano.
(i) Shirika linatoa fursa kwa taasisi binafsi na za umma kuwekeza kwa ubia katika maeneo ambayo DDC inamiliki katikati ya Jiji hivyo kukufanya kuwa sehemu na mmiliki wa majengo na vitega uchumi katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
(ii) Shirika linatoa fursa kwa watu kupata vibanda vya maduka, kumbi za burudani, baa, migahawa, ofisi na maeneo ya kukodi ili kufanya biashara katikati ya Jiji la Dar es Salaam hivyo kuchochea kukua kwa uchumi wa Jiji na nchi kwa ujumla.
(iii) DDC inaamini katika ushirikishwaji kama nyenzo muhimu ya kuboresha mipango na shughuli za Shirika hivyo mawazo yako ni muhimu ili tufikie malengo yetu ya kuinua uchumi wa Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 2128800
Namba ya Mkononi:
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.