• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Halmashauri ya Jiji la DSM yaadhimisha Wiki ya Upandaji Miti kwa lengo la kutunza mazingira

Posted on: March 25th, 2025

Na: Doina Mwambagi

 Katika kuadhimisha Wiki ya Upandaji Miti, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeendelea kutekeleza juhudi za uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mpango endelevu wa kuhakikisha mazingira yanabaki salama kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Maadhimisho hayo ya wiki ya upandaji miti yamefanyika Leo tarehe 25 Machi 2025 katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko iliyopo Jijini humo.

Akiongea  na wanafunzi, walimu na wadau wa mazingira mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Kishe Adrian amesema anatambua jitihada zinazofanywa na Halmshauri ya Jiji la Dar es salaam katika kutunza mazingira kwa kuhamasisha wananchi matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupanda miti

“Nawasihi tuendelee kutunza miti tuliyoipanda kwa sababu ni urithi wa kizazi kijacho. Tunapanda miti leo kwa ajili ya mustakabali wa baadaye.” Ndg. alisema Kishe.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi Tabu Shaibu  amesema Katika kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inaendelea kusisitiza umuhimu wa upandaji na utunzaji wa miti kwa manufaa ya sasa na ya baadaye. Kupitia kaulimbiu “Ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa rasilimali kwa kizazi hiki na kijacho,” Jiji limejizatiti kuhakikisha miti inapandwa na kuhifadhiwa si tu kwa ajili ya kutoa hewa safi, bali pia kwa kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na misitu kama mbao, matunda, na mimea dawa. Jitihada hizi zinahakikisha kuwa rasilimali za misitu zinatumika kwa uangalifu, huku kizazi cha sasa kikifaidi na pia kuwaachia urithi endelevu wale watakaokuja baadaye.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mkuu wa kitengo cha  maliasili na uhifadhi wa mazingira Bi Teresia Denis amesema  Halmashauri ya Jiji kwa miaka mitatu 2022-2025 imefanikiwa kupanda miti  zaidi ya 2,149,601 katika maeneo mbalimbali ikiwemo shule, magereza, bonde la moto msimbazi na ufukweni.

Halmashauri ya Jiji imeahidi kuendelea kutekeleza mpango huu ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali, huku ikiwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika juhudi hizi za kutunza mazingira kwa faida ya vizazi vijavyo.

Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.