Na: Shalua Mpanda
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amesema Serikali inakusudia kuweka kamera za usalama katika maeneo tofauti katika Jiji hili ili kuwezesha wafanyabiashara na Wananchi kufanya shughuli zao mchana na usiku.
Ameyasema hayo leo wakati wa utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya ufungaji wa taa 213 za barabarani na kampuni ya M/S EH Enginerring Company Ltd.
Mabelya amesema ufungaji wa taa smbamba na kamera hizo za barabarani ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mkoani Dar es Salaam.
"Tunakamilisha taratibu za ufungaji wa kamera katika eneo la kuzunguka Soko la Kariakoo na makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru na Uhuru na Lumumba". Alisema Mkurugenzi huyo
Aidha, Mkurugenzi Mabelya amebainisha kuwa Halmashauri ya Jiji lina uhitaji wa taa 37,847 kwenye mitaa 159 yenye barabara zenye urefu wa kilomita 1,135.405 na mpaka sasa tayari taa 2,238 na kati ya taa hizo taa zinazotumia sola ni 1,926 na taa za umeme ni 312.
Utiaji wa saini wa mkataba huo umeambatana na zoezi la uzinduzi wa uwashaji wa taa za barabarani katika eneo la soko la Machinga lililopo Karume.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.