Na: Shalua Mpanda
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi na Watendaji wengine kushuka chini na kwenda kutatua kero za Wananchi.
Ametoa agizo hilo katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa shule za Sekondari Nchini katika shule maalum ya wasichana ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Amesema si busara viongozi wa Serikali kukaa ofisini wakati wananchi wana changamoto mbalimbali katika maeneo yao hivyo amewataka viongozi hao kwenda kuwahudumia.
“Haipendezi kukaa ofisini wakati wananchi wana matatizo,shukeni chini katatueni kero za Wananchi , Ofisi za Wakurugenzi hamuwezi kukosa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto ndogondogo za wananchi”. Alisema Mchengerwa
Aidha, ameitaka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanamaliza kero za barabara ambayo imekuwa changamoto na kilio kikubwa kwa Wananchi katika maeneo mengi Nchini.
Katika hafla hiyo, shule 7 za Mkoa wa Dar es Salaam zilikabidhiwa vya TEHAMA zikiwemo kompyuta mpakato n.k.kati ya shule 100 za nchi nzima zilizopokea vifaa hivyo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.