Waziri Mkuu Mstaafu na Mshauri wa Rais katika masuala ya kilimo, Mhe. Mizengo Pinda, ametoa wito kwa viongozi wa Kanda ya Mashariki kuboresha maonesho ya Nane Nane kwa ubunifu na ubora ili kuwanufaisha wakulima, wafugaji na wavuvi.
Akizindua maonesho hayo katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Morogoro, Mhe. Pinda alipongeza ushirikiano wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga chini ya uratibu wa Mkoa wa Morogoro, akisema yanaakisi juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuendeleza sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Amesisitiza taasisi za udhibiti kama TBS na TFDA kushiriki kikamilifu kusaidia bidhaa za wajasiriamali, huku vyuo kama SUA vikitakiwa kutoa elimu ya kitaalamu kwa wananchi.
Kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Mashariki, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Aboubakari Kunenge, amesema maonesho hayo yanaonyesha mafanikio ya Serikali kwa vitendo kupitia matumizi ya teknolojia.
Mhe. Pinda alihitimisha kwa kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kwa kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, akisisitiza kauli mbiu ya mwaka huu:
"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.