Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 31 Agosti, 2023 limefanya kikao chake cha kawaida cha kupitisha na kujadili taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2023.
Kikao hicho kilichoongozwa na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam kiliweza kupitia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Fedha na Utawala, Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira pamoja na Kamati ya Kuthibiti UKIMWI kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2023 lengo likiwa ni kujiridhisha juu ya utendaji kazi wa kamati hizo.
Sambamba na hilo, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira kupitia Divisheni ya Miundombinu Kamati imeweza kusimamia ukaguzi na utoaji wa vibao vya ujenzi vipya 182 na vibali 74 vya ukarabati huku Idara ikitoa notisi 44 kwa watu waliojenga bila ya kuwa na vibali vya ujenzi pamoja na kutatua migogoro ya Ardhi na mipaka katika Mitaa na Kata mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Akitoa maelekezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Mbala Shitindi amesema “Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni Taasisi ya Bima ya Afya ya Jamii iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Taifa ya Bima ya Afya, Sura ya 395 kwa lengo kuu la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa watu”.
Aidha, Bw. Shitindi ameendelea kusema Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) una kifurushi cha mafao ya kuvutia ambacho hutolewa kwa walengwa wake kupitia vituo vya afya vilivyoidhinishwa nchini kote. Mfuko huu una jumla ya mafao kumi na moja (11) ambayo hutolewa kwa walengwa kulingana na Miongozo ya Kawaida ya Tiba iliyotolewa na Wizara ya Afya pamoja na kanuni za Mfuko huku akieleza baadhi ya magonjwa ambayo Bima ya Afya haigharamikii kwakua ziko chini ya Serikali ikiwemo matibabu ya Kifua Kikuu pamoja, Chanjo pamoja na huduma nyingine ambazo hazipo kwenye kifurushi husika.
Pia, Bw. Shitindi ameeleza Baraza la Madiwani kuwa kwa upande wa Vifurushi ambavyo havipo kwenye kifurushi cha muhusika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wanajukumu la kuingia Mkataba na Mwajiri ili kuweza kubadilisha kifurushi.
Aidha, Baraza liliridhia na kupitisha taarifa hiyo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.