Idara ya Maendeleo ya Jamii leo tarehe 28 Novemba 2022 imetoa mafunzo ya kwa Watendaji wa Mtaa kutoka Jimbo la Ukonga lililopo ndani ya Halmashairi ya Jiji la Dar es Salaam katika uKumbi wa mikutano Anatoglou uliopo Mnazi Mmoja Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Francisca Makoye akiwa anatoa maelekezo katika kikao kazi cha mafunzo hayo amesema.
"Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inasimamia na kutekeleza mpango wa serikali juu ya utoaji mikopo inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu"
Mfumo huu ni mfumo wa usajili na utoaji wa mikopo itokanayo na aslimia kumi 10% ya mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu (TPLMIS).
Mafunzo hayo yamelenga kutoa ufahamuna kwa watendaji hao ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kiurahisi wakiwa na uelewa na weledi katika shughuli mbali mbali ya kijamii.Huku malengo makuu ni kutoa mafunzo juu ya ufahamu wa mfumo wa kusajiri vikundi vya wajasiriamali,kufahamu uratibu wa wa mashirika yasiyo ya kiserikali namna ya usajili wake na masharti katika usajili huo na kufahamu taarifa za mikopo kwa kila kikundi sambamba na mwenendo wa urejeshwaji wake.
Watendaji wa mtaa ni wadau na watumishi wa serikali wanaohudumu katika Jimbo la Ukonga ndani ya Halmashairi ya Jiji laDar es salaam ni wadau muhimu kufahamu na kuelewa mifumo hii ili kueleza vyema wakati wakikutana na wanachi na kuwapa taarifa kuhusu mikopo inayotolewa na serikali kwa makundi ya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Aidha,kuongeza ufanisi wa utoaji huu wa mkopo ni lazima watu wote washirikiane kufahamu namna gani mikopo hii inanufaisha wananchi wote kwa usahihi.
"ni muhimu tufahamu kuwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali lazima yasajiliwe katika hili watendaji wa mtaa ni muhimu kujua katika mtaa wako mashirika yote yamesajiliwa kwa kushirikiana na afisa maendeleo ya jamii katika kata kutekeleza hili"
Mwakilishi kutoka ofisi za usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali.Vile vile kikao kimeazimia kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo kutoka katika vikundi vyote kwa mipango kazi ambayo kwa mwaka mara nane kukutana na vikundi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.