Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii jijini Dar es Salaam kinapatikana katika jengo la kale la Old Boma ambalo lina zaidi ya miaka 160.
Jengo la Old Boma linalomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lina historia kubwa katika nchi yetu limefanyiwa ukarabati kwa kiwango cha juu na kuwa mfano wa uhifadhi endelevu na kituo cha kutangaza historia ya ukuaji wa miji yetu kanda ya Afrika Mashariki kwa ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya.
Lengo la kuanzisha Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wabunifu Majengo Tanzania, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ni kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kutunza na kudumisha majengo ya kale ambayo yatakua yakisaidia kukuza na kuendeleza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.