Na: Doina Mwambagi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, amesema kuwa Serikali haitavumilia mtu yeyote atakayefanya hujuma, uzembe, au vitendo vya jinai katika utekelezaji wa miradi ya elimu.
Ametoa kauli hiyo leo Disemba 22, 2025, wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kitunda Relini, iliyopo Kata ya Kitunda wilayani Ilala.
Naibu waziri huyo wa TAMISEMI amesisitiza kuwa Serikali inawekeza kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuhakikisha watoto wote wa Kitanzania wanapata elimu kwa wakati na katika mazingira bora.
Amesema kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya ya wale watakayehujumu jitihada hizo.
"Elimu ni urithi wa watoto wetu, na Serikali haitavumilia yeyote atakayefanya hujuma katika sekta ya elimu," Alisema.
Aidha, Mhe. Kwagilwa ametambua jitihada za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuongeza fedha kutoka mapato yake ya ndani na kujenga shule hiyo ya kisasa, jambo linaloongeza upatikanaji wa elimu kwa watoto wa Kitanzania.
Pia amezitaka Halmashauri nyingine nchini kuiga mfano huu kwa kutumia mapato yao ya ndani katika ujenzi wa shule bora na za kisasa.
Ziara hiyo ina lengo la kuhakikisha miradi ya elimu inatekelezwa kwa ufanisi, kwa kuzingatia thamani ya fedha, na kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.