Wednesday 22nd, January 2025
@Vituo vya Kupigia Kura Tanzania Bara
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 ibara 4(1-3) (Matangazo ya Serikali Na. 371, 372, 373 na 374) ya mwaka 2019, Waziri mwenye dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anautangazia umma wa Watanzania na Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu kuwa tarehe 24 Novemba, 2019 itakuwa ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara. Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani S. Jafo (MB.) anawatakia uchaguzi mwema, amani na utulivu katika kipindi chote cha uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na upigaji kura.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.