Na: Shalua Mpanda
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa George Simbachawene amewasihi watanzania kudumisha amani na kutoruhusu watu wachache kuvuruga kuvuruga amani hiyo.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Vingunguti katika "Usiku wa Nyamachoma" ulioandaliwa na Diwani mteule wa Kata hiyo Omary Kumbilamoto katika Soko la Nyamachoma-Kumbilamoto jana.
Mhe. Sinbachawene amewataka wakazi hao wa Vingunguti na watanzania kwa ujumla kutokukubali kugombanishwa kwa itikadi za vyama, dini au matabaka bali watangulize maslahi ya Nchi kwanza.
"Amezungumza hapa mheshimiwa Diwani Kumbilamoto kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa gharama kubwa, halafu kinatokea kikundi cha watu wanaenda kuiharibu, hizi ni kodi zetu wenyewe na tutakuja kuwabebesha mzigo wa madeni watoto wetu na vijana wetu baadae". Alisisitiza
Awali akimkaribisha Mhe. Waziri, Diwani mteule wa kata ya Vingunguti Mhe. Kumbilamoto alimueleza Waziri huyo kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imetekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo kwa kipindi cha utawala wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo wananchi hawana budi kuitunza miradi hiyo huku akiwataka kudumisha amani kwa kuwa ndio sifa kuu ya watanzania.
Usiku huo wa nyama choma ulisindikizwa na burudani mbalimbali ambapo Waziri huyo wa Mambo ya Ndani alishiriki burudani hiyo na kuwa kivutio kwa wakazi hao wa Vingunguti.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.