Wednesday 15th, January 2025
@Bustani ya Kaburi Moja iliyopo mkabala na Benki ya NBC iliyopo Mtaa wa Samora
Uzinduzi wa Mradi wa Maboresho ya Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam ambao umefadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia JICA ambao umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani 400,000 na ulioanza kutekelezwa mnamo mwezi Januari, 2017 na umekamilika mwezi Agosti, 2017.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya mifano ambayo imeandaliwa kwa pamoja na wataalam wa JICA na wa Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania zinazojihusisha na usafiri/usafirshaji katika Jiji la Dar es Salaam.
Wageni mbalimbali wakiongozwa na mgeni rasmi, Mhe. Paul C. Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka Taasisi zinazojihusisha na usafiri/usafirshaji katika Jiji la Dar es Salaam wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo muhimu.
Kukamilika kwa Mradi huu ni mwanzo wa maandalizi ya Kitabu cha Mwongozo wa Maboresho/ujenzi wa barabara za Mitaa ya Jiji la Dar es Salaam na Miji mingine nchini Tanzania "Urban Street Design Manual" kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.