Monday 6th, January 2025
@Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo na Karakana Mwananyamala
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inapenda kuwajulisha wananchi kwamba kuanzia tarehe 16-23 Juni, mwaka huu, Jiji la Dar es Salaam linaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika nchini kote. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yakiwa na Kauli mbiu: "Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi."
Katika maadhimisho hayo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inawakaribisha wananchi katika maonesho ya wajasiriamali katika Viwanda Vidogo Vidogo vya Halmashauri ya Jiji vilivyopo eneo la Mwananyama katika Manispaa ya Kinondoni, jirani na Hospitali ya Mwananyamala kuona kazi zinazofanywa na wajasiriamali hao ambao ni wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pia inapenda kuwajulisha wananchi kwamba Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam tarehe 19 Juni, mwaka huu kuanzia saa 03:00 asubuhi atakuwa katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kuwajulisha wananchi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mabasi katika eneo la Mbezi Luis ambako huduma za usafiri wa ndani na nje ya nchi zitahamishiwa kutoka Kituo cha sasa cha Ubungo.
Tafadhali usikiapo taarifa hii mjulishe na mwingine na shiriki bila kukosa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.