Meneja wa NMB tawi la Airport Bw. Restus Asenga kwa niaba ya Mgeni rasmi Bw. Dismas Prosper ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam amewaahidi Walimu pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Juhudi kutatua changamoto ya Madawati na Kompyuta wanayoikabili shuleni humo.
Hayo ameyasema alipokua akizungumza katika Mahafali ya 19 ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Juhudi yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo iliyopo Gongolamboto Jijini Dar es Salaam.
Bw. Asenga amesema Bank ya NMB imekua na mchango mkubwa katika kuhakikisha wanaboresha elimu katika shule za Msingi na Sekondari kwa kurudisha faida zao kusaidia jamii kwani Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya juhudi kibwa sana katika kuhakikisha Sekta ya elimu nchini inakua kwa kasi zaidi.
“Elimu ni msingi mzuri wa mwanafunzi kuboresha maisha yake, sisi kama NMB imekua niutamaduni wetu kurudisha faida kwa jamii kwa kuhakikisha tunasaidia sekta ya elimu kuendeleakukua kwa kasi hivyo kwa niaba ya Meneja wa Kanda NMB Bank tunaahidi kushirikiana na walimu kusukuma gurudumu hili kufika linapohitajika hivyo niwaahidi changamoto za upungufu wamadawati pamoja na kompiuta tumelipokea na tutalitatua kwa wakati.”
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa Shule ya Sekondari Juhudi Mwl. Happiness Pallangyo amewaahidi wazazi na walezi kuwa kwa maandalizi waliyoyafanya kuwaandaa wanafunzi ni matumaini yao kuwa Wanafunzi hao wanaokwenda kuhitimu watafanya vizuri katika mitihani wao wa kumaliza elimu ya sekondari inayotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 13, 2023 huku akimuahidi mgeni rasmi kusimamia Kikamilifua taaluma, nidhamu na michezo lengo likiwa ni kutekeleza adhma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha Sekta ya Elimu inakua bora zaidi.
Sambamba na hilo Mwl. Pallangyo ameweza kushukuru viongozi wote wa Mkoa wa DSM, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, viongozi wa Tarafa, Kata na Mitaa pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo NMB Bank, Letshego Bank, vyombo vya Ulinzi na Usalama ,TBA, CAMFED na wafadhili kutoka Marekani (SPY BASKETBALL ACADEMY) kwa mchango wao mkubwa wa kuhakikisha maendeleo ya Shule ya Sekondari Juhudi yanakua kwa kasi katika kila sehemu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.