Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imefanya ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2022/2023 (Oktoba hadi Desemba2022) Ambapo walitembelea Shule za Sekondari Viwege na Mvuti na Shule ya Msingi Kigogo Fresh.
Akizungumza kwenye ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma zaJamii Mhe. Robert Manangwa ameeleza kuwa wameridhishwa na Ubora wa shule na kumpongeza Kaimu Mkurugenzi pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa usimamizi wa fedha za Serikali.
Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari Viwege iliyopo Kata ya Majohe Bi. Kalunde Sigera ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha miundombinu katika shule hiyo ambapo amebainisha kuwa katika shule yake kuna miradi minne ambayo tayari imetekelezwa kwa mwaka 2022/2023 ambayo ni ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, ujenzi wa bwenj la Wasichana, jengo la Utawala pamoja na Maabara mbili ya Baiolojia na Kemia.
"Shule ilipokea Shilingi Milioni 120 kutoka Serikali Kuu maarufu kama ‘Pochi ya Mama’ kwa ajili ya ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, kiasi cha Sh. Milioni 118.9 zimetumika kujenga vyumba sita vya madarasa, Ofisi mbili za walimu, Madawati, Viti na Mezatumepata 30 pia tumelipia service line ya TANESCO ili jengo hili liwe na umeme wake peke yake ambao utaunganishwa pia kwenye Jengo tunalolijenga la maabara" Amesema Bi. Karunde.
Vilevile Bi.Kalunde ameongeza kwa kubainisha fedha walizopata kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo ni sh. Milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la Wasichana na fedha iliyotumika ni sh.Milioni 51.5 ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 28 Machi 2023, Ujenzi wa Jengo la Utawala umepokea sh. Milioni 65 kutoka mapato ya ndani na mpaka sasa imetumika sh. Milioni 31.7 ambao ujenzi huo nao unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 28 machi 2023 sambamba na sh. Milioni14 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Maabara baada ya Maabara iliyokuwepo kuungua.
Kwa upande wake Mwl. Gasper Mwaipopo Mkuu wa Shule ya Sekondari Mvuti naye amemshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi huo ambao umetoa fursa kwa wanafunzi kupata elimu iliyo bora pamoja na viongozi wengine ambao wameshiriki vyema na kubainisha miradi miwili ambayo wameitekeleza katika shule yake 2022/2023 ambao ni mradi wa Bweni unaoendelea pamoja na Mradi wa Pochi ya Mama ambao umejikita katika ujenzi wa madarasa tisa ulioanza tarehe 3 Novemba na kuthibitisha mpaka sasa Mradi huo tayari umekamilika kwa asilimia 100
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.