Na: Hashim Jumbe
CHAMA cha Wanasheria watetezi wa mazingira (LEAT) leo tarehe 15 Aprili, 2021 wamekutana na wadau wa uhifadhi wa mazingira kutoka katika Wilaya Tano (5) za mkoa wa DSM na kujadiliana changamoto za kimazingira zilizopo kwenye Wilaya hizo na kisha kutoa mapendekezo ya namna ya kuzitatua changamoto hizo.
"Leo tupo katika mzunguko wetu wa pili wa kuunda timu ambazo zinakwenda kutembelea maeneo yenye changamoto za kimazingira, kwa hivyo tumekutana na Wilaya zote Tano (5) za mkoa wa DSM, lengo likiwa ni kuunda timu zitakazokwenda kutembelea maeneo hayo na kutafuta ufumbuzi ya nini kifanyike ili kuondokana na changamoto kwenye maeneo hayo" Teresia Fabian-Afisa Mradi LEAT
Itakumbukwa kuwa LEAT ni asasi isiyokuwa ya Kiserikali inayosimamia sheria za mazingira, ambayo kwa sasa inatekeleza mradi wa miaka miwili wa uhifadhi wa mazingira kwenye mkoa wa DSM na kaulimbiu yake ni 'kulinda haki za kimazingira kwa wanawake, vijana, wasichana na jamii kwa ujumla kupitia kuwezesha jamii katika masuala ya kisheria Jijini DSM'
Aidha, kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la DSM teyari LEAT kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri, Madiwani wa Kata za Pugu na Mnyamani pamoja na Wenyeviti wa Mitaa yao, wameweza kupatiwa elimu ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kutembelea maeneo yenye changamoto na kutolea mapendekezo.
Katika awamu ya pili ya mradi huo, teyari LEAT na wadau wa Halmashauri ya Jiji la DSM wamepanga kutembelea Mitaa Mitatu (3) ya Kata ya Liwiti ambayo imekumbwa na athari za mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, ziara hiyo itafanyika tarehe 20 Aprili, 2021
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.