Na; Judith Msuya na Miraji Omary.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla, leo Septemba 1, 2021 amesimamisha michango yote wanayotozwa Wanafuunzi wa Shule za Msingi na Sekondari mpaka hapo ambapo utaratibu utakapo fuatwa wa kuwashirikisha Wananchi nayeye kuridhia.
Maelekezo hayo ameyatoa baada ya kupokea kero za Wananchi kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Segerea ambao Wazazi wamedai wamekuwa wakichangia kiasi cha Shilingi 300 hadi Tsh 1,000 kwaajili ya gharama za uchapaji wa Mitihani pamoja na masomo ya ziada ambayo ni kinyume na waraka wa Elimu bure ambapo imeonekana wazazi na walezi kushindwa kuhimili michango hiyo
Aidha, Mhe. Makalla amesisitiza kuwepo na maridhiano baina ya Wazazi na Walimu juu ya michango inayotolewa Shuleni endapo wakiridhia michango hiyo watume maombi kwa ofisi za Mkuu wa Wilaya ili ziweze kuidhinisha michango hiyo."Kama wazazi au walezi wamekubaliana na walimu na kuitishwa mkutano, wazazi hao wanatakiwa kuorodhesha majina yao pamoja na kuweka sahihi kwamba wamekubali Watoto wao wasome masome ya ziada au wale chakula cha shule, tupo tayari barua hizo zinakuja na zipitie kwa Mkuu wa Wilaya ili ziweze kunifikia na mimi nitapitisha ilimradi wananchi washirikishwe na mimi nitaidhinisha ili muendelee kusudi tuepushe kero ndogondogo zinazojitokeza baina yetu na wananchi wetu."Amesema RC Makalla
Sambamba na agizo hilo lakini pia Mkuu wa Mkoa ameelekeza kuwa kwakua kuna uhaba wa ardhi katika maeneo mengi ya Shule hivyo fedha zinazotolewa kwaajili ya ujenzi wa madarasa zitumike kujenga madarasa ya juu kusudi eneo dogo liweze kujenga madarasa yakutosha. "Tumeamua fedha zote zinazotolewa kwaajili ya mradi wa ujenzi wa Shule zitumike kujenga madarasa ya juu ili tutumie eneo dogo ambalo litaweza kutoa madarasa mengi na yatakayowatosha wanafunzi wengi zaidi hayo ndio maelekezo yangu kwa Ofisi ya Mkurugenzi".
Naye Afisa Elimu Takwimu na Vielelezo Bi.Wema Kajigili ameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ikiwemo suala zima la kusitisha michango kwa wanafunzi hadi utaratibu mwingine utakapotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.