Na: Shalua Mpanda - Zanzibar
Wataalamu kutoka Idara ya Mipango na Uchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam , Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamekutana kujadili tathmini ya Hesabu za Fedha za Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa miaka mitano kuanzia 2015/16 hadi 2022/23.
Kikao hicho cha tathmini kilichoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Uchumi wa Afrika (UNECA) kimefanyika leo Februari 11,2025 katika leo hoteli ya "Hotel Verde" mjini Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine, wataalam hao wamejadili namna ya kuzitumia takwimu zilizopatikana katika taarifa za mradi wa "DA-15"(Development Accounting Project 15) ili kuboresha huduma mbalimbali za kijamii katika Halmashauri ya Jiji hili.
Tathmini hii ina lengo la kuona jinsi changamto mbalimbali zilizojitokeza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwemo ugonjwa wa COVID-19 ulivyochangia katika kuchelewesha uboreshaji wa huduma za Jamii.
Mbali na wataalam hao, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alimuwakilisha Mkurugenzi wa Jiji katika kikao hicho.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.